Mwanaume Wa Miaka 30 Amuoa Kwa Nguvu Binti Wa Miaka 14 Simanjiro

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





Jeshi la Polisi mkoani hapa linamshikilia Mwanaume mmoja mkazi wa kijiji cha Loswaki wilaya ya Simanjiro aliyejulikana kwa jina Lalahe Karoli (30) kwa tuhumza za kumtorosha na kwenda kuishi kinyumba na mtoto mwenye umri wa Miaka 14 kwa ridhaa ya Baba wa Mtoto.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara Benjamin Kuzaga amethitisha tukio hilo ambapo amesema mbinu iliyotumika ni mtuhumiwa kumtorosha binti huyo na kumpeleka chumbani kwake na kumlazimisha kufanya nae ngono kisha kuishi nae kwa nguvu.

Kamanda Kuzaga amesema kwa kushirikiana na timu ya upelelezi na raia wema walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo kwa mahojiano zaidi.

Pia Jeshi hilo limeeleza kuwa limemkamata Baba wa Mtoto aitwaye Lembris Salonic (60) mkazi wa Loswati Terati wilaya ya Simanjiro ndiye aliyeidhinisha kuolewa kwa binti yake huyo.


 
Kamanda Kuzaga ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi hilo kutoa taarifa ili kupambana na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na watoto ambavyo vinarudisha nyuma Maendeleo ya mtoto na jamii kwa ujumla.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad