Dully Sykes "Pesa Zangu Ziliishia Kwenye Starehe

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



LEJENDARI wa Bongo Fleva, Dully Sykes anasema kuwa, sababu za wasanii wengi wa zamani kufulia au kutofanikiwa kulitokana na kuendekeza starehe.


Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Dully anasema kuwa, zamani wasanii walikuwa wanapata pesa japokuwa hazikuwa nyingi kama wanazopata wasanii wa sasa, lakini walikuwa wanashindwa kufanya vitu vya maana zaidi ya starehe.


“Tulikuwa tunapata pesa ambazo kama tungetumia akili ya kuzidunduliza tungeweza kununua viwanja vitatu hata vinne ambavyo kwa miaka ya sasa mtu angeweza kuuza hata kimoja tu ukajenga nyumba, lakini hatukufanya hivyo zaidi sana pesa ziliishia kufanya starehe,” anasema na kuongeza;


“Hata ukifuatilia nyimbo zetu tulizokuwa tunaimba zamani zilikuwa zinahamasisha starehe, kula vizuri na kuvaa vizuri tofauti na sasa ndoto za wasanii wengi ni kujenga nyumba na kumiliki magari mazuri.”


Dully anasema pesa walizokuwa wanapata kipindi hicho cha nyuma zilikuwa zinawatosha, lakini zilikuwa hazina matumizi sahihi hivyo wakongwe hawatakiwi kuwa na sababu kwamba walikuwa hawapati pesa na kufanya mambo makubwa.


Mkali huyo wa ngoma ya Salome anasema kuwa, hakuna pesa ndogo, bali muhimu ni kuwa na malengo na utafanikiwa tu.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad