Harmonize Hajawahi Nipe Hata Shilingi Sifuri Kutoka Wimbo wa Attitude, Hela Kubwa Aliyowahi Nipa ni Milioni 2 ili Nikapange

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Officially imejulikana wazi sababu za msanii @h.baba_ kujitenga na Konge Gang,na hii ni kutokana na sauti ya msanii huyo kunaswa kwenye vimbweta vya wambea chini ya @soudybrown , sauti hiyo ya msanii H. Baba kupitia U-HEARD ya XXL (Clouds FM), imesikika na kufunguka mengi yaliyofanya ajitenge na Konde Gang.


H. Baba amedai toka wimbo wa Attitude uachiwe, hajawahi pokea hata senti sifuri kutoka kwenye mapato ya wimbo huo, lakini pia amefungiwa hadi show na hawezi Kuperform wimbo huo. H. Baba ameendelea akisema pesa kubwa ambayo amewahi pewa na msanii @harmonize_tz ni shilingi milioni 2 ambazo aliambiwa akapange. Huku rais huyo wa Mwanza akishangaa unapangaje Dsm kwa milioni mbili,kwenye pesa hiyo hiyo ununue vitu vya ndani.


H. Baba ameendela kuongea kuwa ametumia pesa nyingi kumpigania Harmonize lakini hajawahi pata faida huku akidai kuna siku alipewa elfu ishirini mbele za watu na kubwa zaidi lililomuuma H. Baba ni Harmonize kuwahi kumtamkia kuwa ana tamaa. H. Baba pia amedai si kuwa Harmonize hana pesa,ila ana mkono wa kukunja.


Kingine msukuma wa Roc City amegusia ishu ya kutokuwepo kwenye List ya wasanii watakao fanya performance kwenye tamasha la Afro East Carnival,akidai anashangaa kutokuwepo, ukizingatia alijichukulia kama mtu wa muhimu wa msanii huyo, kwenye List mbili zote katemwa. Cha mwisho H Baba amedai amechoka kuteseka na ameamua arudi Mwanza maana ana kila kitu huko kuanzia nyumba na magari kuliko kuendelea kupanga Dsm bila maslahi.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad