Rais Samia azindua daraja la Tanzanite kumuenzi Magufuli

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Dar es Salaam.  Rais Samia Suluhu Hassan amesema uzinduzi wa mradi wa daraja la Tanzanite ni sehemu ya kumuenzi Rais wa awamu ya tano, John Magufuli.

Ameyasema hayo leo Alhamisi Machi 24, 2022 Dar es Salaam kwenye hafla ya uzinduzi wa daraja hilo lilogharimu Sh243 bilioni.

Rais Samia amesema Desemba 20/2018 aliyekuwa Rais Hayati Magufuli aliweka jiwe la msingi kwa ajili ya kuanza ujenzi huo na kueleza kwamba ni siku ya furaha kuona kazi aliyoianzisha imekamilika.

“Na tumekusanyika hapa kwa ajili ya uzinduzi na kama nilivyosema mara kwa mara kwamba tutakamilisha kazi zote alizozianzisha kwahiyo kwangu mimi uzinduzi wa daraja hili ni sehemu ya kumuenzi Rais John Magufuli,”amesema


 
Rais Samia amesema serikali ya Korea Kusini ni mdau mkubwa wa maendeleo ambaye amekuwa akiwaunga mkono katika sekta mbalimbali za kimaendeleo hususan kwenye miundombinu.

“Kwaniaba ya wananchi wa Tanzania napenda kutoa shukrani kwa Jamhuri ya Korea ya Kusini kwa mchango wao mkubwa wa maendeleo katika Taifa letu,”amesema

Amesema ujenzi wa daraja hilo ni muendelezo wa Serikali katika kufanya maboresho kwenye sekta ya miundombinu ili kukabiliana na kero ya msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.


“Kwa kufanya upanuzi wa barabara za juu na miundombinu ya mabasi yaendayo haraka ili kurahisha usafiri ndani ya jiji la Dar es Salaam,”amesema
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad