4/12/2022

Masau Bwire “Nilikuwa nafanya kazi ya kuisemea Ruvu Shooting Kwa kujitolea, nilikuwa silipwi"


“Nilikuwa nafanya kazi ya kuisemea Ruvu Shooting Kwa kujitolea, nilikuwa silipwi hata senti, wakati fulani Timu inasafiri kwenda mkoani mimi nasafiri nayo kwa gharama zangu Kwa yale mapenzi kwamba naguswa na naipenda Timu.

“Ikafika wakati Mwenyekiti wa Timu na Mkuu wa Kikosi Cha 832 Ruvu JKT, Alikuwa Charles Mbuge, Meja Jenerali, ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera akaniita akaniambia haiwezekani tusikupe chochote “Hebu Tuambie tukulipe kiasi gani ?” Nikawaambia sielewi ofisi yako na wewe mwenyewe mnauwezo kiasi gani na mnaweza kunilipa kwa Namna Gani, kwa hiyo Mimi nawaachieni kile mnachoweza mtakachoona kinafaa basi mimi nitashukuru Mungu.

“Siku hiyo hiyo baadaye ilikuwa ni siku za mwanzo wa Mwezi nikapigwa mshiko, kwa hiyo kuanzia hapo mpaka sasa nikawa kwenye mfumo wa malipo,” @masaubwire 

#WasafiSports

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger