Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) Sheikh Khalifa bin Zayed Al Nahyan amefariki


Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) Sheikh Khalifa bin Zayed Al Nahyan amefariki, shirika la habari la Imarati WAM limeripoti muda mfupi uliopita na kusema amefariki akiwa na umri wa miaka 73.

"Wizara ya Masuala ya Rais ilitangaza kuwa kutakuwa na siku 40 za maombolezo rasmi na bendera nusu mlingoti na siku tatu kufungwa kwa Wizara na Mashirika rasmi katika ngazi ya shirikisho na Serikali za mitaa na sekta ya kibinafsi” taarifa imeeleza.

Sheikh Khalifa ambaye amekuwa akiugua kwa miaka kadhaa kulikosababisha kwa muda mrefu aache kujihusisha na shughuli za kila siku alimuachia mikoba kaka yake ambaye ni Mwanamfalme wa Abu Dhabi Mohammed bin Zayed ambaye ndiye ameonekana kama Mtawala kwa muda huo.

Sheikh Khalifa ambaye ni nadra kuonekana kwenye picha rasmi au kwenye hafla za umma kwa miaka mingi, alimrithi Baba yake na Mwanzilishi wa UAE Sheikh Zayed mnamo mwaka 2004, alipata kiharusi muongo mmoja baadaye na kumweka mbali na Watu tangu wakati huo.

đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

đŸ’¥NAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad