Simba Yatoa Taarifa kwa Umma Kuhusu Hatima ya Bernard Morrison

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPASimba imempatia mapumziko ya hadi mwisho wa msimu mchezaji wao Bernard Morisson

KLABU ya soka ya Simba imeuarifu Umma hasa mashabiki wake na wapenzi wa soka nchini kuhusu hatima ya mchezaji wao Bernard Morrison.

 

Katika taarifa yao iliyochapishwa kwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Instagram wa klabu hiyo imeonesha mchezaji huyo amepewa likizo ya mapumziko hadi mwisho wa msimu ili kumpatia nafasi ya kushughulikia matatizo binafsi.

 

Sambamba na hilo Simba imemshukuru Morrison kwa muda wote alioitumikia klabu hiyo ikiwa ni pamoja na kuisaidia klabu hiyo kupata makombe kadhaa likiwemo kombe la Mapinduzi, Kombe la Shirikisho la Azam Sports, Ubingwa wa Tanzania Bara pamoja na kuisaidia klabu hiyo kufika robo fainali ya michuano ya Afrika mara mbili.Bernard Morrison mchezaji raia wa Ghana amekuwa na matatizo kadha wa kadha na mengi yakiwa ni matukio ya nje lakini pia vitendo vya utovu wa nidhamu imekuwa ni sehemu ya mambo yanayomuandama licha ya kwamba ni moja kati ya wachezaji wenye kiwango cha hali juu katika kusakata kabumbu.

 

Kumekuwa na taarifa zinazoendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimhusisha kujiunga na waajiri wake wa zamani klabu ya Yanga.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad