Mwanamuziki Jose Chameleone Atoa Masharti ya Kuuzika Mwili Wake: "Kama si Jeneza la Glasi Msijaribu"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



 
Mwanamuziki Jose Chameleone ametoa maagizo kuhusu safari yake ya mwisho duniani akitaka kuzikwa kwa jeneza la vioo
Chameleone vilevile amesema kuwa kifo chake kitatengeneza pesa nyingi ajabu ambazo anataka apewe mgao wake kufaidi akiwa hai

Msanii huyo anatambulika kwa vibao mbalimbali kama vile Mama Mia, Valu Valu, Tubonge, Jamila na Bwerere

Mwanamuziki matata kutoka taifa la Uganda Jose Chameleone ameanza kujipanga kwa safari yake ya mwisho duniani.

Ninataka Kutengeneza Pesa Nyingi Sana kutoka kwa Kifo Changu, Msanii Jose Chameleone Asema
Mwanamuziki mashuhuri kutoka taifa la Uganda Jose Chameleone. Picha: Jose Chameleone.
Mwanamuziki huyo anadai kuwa haogopi kuaga dunia akisema kuwa ananuia kufaidika kutokana na kifo chake.

Kwenye mahojiano na runinga ya NBS ya Uganda, Chameleone amesema kuwa maziko yake yatatengeneza kiasi kikubwa cha fedha akiwataka wasimamizi wa maziko ambayo wanania ya kusimamia maziko yake kuwasiliana naye.

Mwanamuziki huyo ambaye anatambulika kwa nyimbo mbalimbali kama vile Tubonge, Valu Valu, Mama Mia na Bwerere anataka wasimamizi hao kummegea sehemu yake ya kipato ili kufaidi akiwa angali hai.


 
Meru: Afisa Mkuu wa Polisi Apatikana Ameuawa Nyumbani kwa Mpenziwe
Kwa mujibu wa Chameleone, meneja wake anajua aina ya ibaada anayotaka mwili wake ufanyiwe atakapofariki akisema kuwa mwili huo uzikwe kwa jeneza la glasi.

Kulingana naye, hilo litasaidia mashabiki wake kuuona mwili wake kwa urahisi kwani halfa ya maziko yake itahudhuriwa na umati mkubwa wa watu.

"Nataka niwe na sanduku la kioo ili kila mtu anione kwa sababu watu wengi watahudhuria mazishi yangu kutoka nchi kadhaa," alisema.

Chameleone vilevile alitoa wito wa muziki wake kuchezwa akiwa hai akiwaambia mashabiki na vyombo vya habari dhidi ya kupiga zaidi ngoma za wasanii wakati wakiwa wameondoka duniani.

“Mimi nilikuwa shabiki wa kwanza wa Mowzey Radio kwa sababu niliona kipaji chake kisha nikamuonyesha nyie watu. Sio sawa kumkumbuka mtu akikufa unapaswa kuwasherehekea wangali hai,” alisema akimkumbuka msanii Mowzey Radio aliyefariki miaka minne iliyopita.

Mapenzi Hayana Mwakenya: Harmonize Amvisha Kajala Pete ya Uchumba
Msanii huyo alikuwa akizungumza katika mahojiano na runinga ya NBS baada ya kurejea nchini kwao Uganda kutoka jinini Kinshasa, Kongo ambako alikuwa na ushirikiano wa kikazi na msanii Koffi Olomide.

Chanzo: TUKO.co.ke
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad