Ticker

6/recent/ticker-posts

Adai hajawahi kugusa kiwashio cha umeme kwa miaka 78


Waziri wa Nishati, January Makamba amefanya mahojiano na Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 78, ambaye amemuambia hajawahi kubonyeza kitife cha kuwasha taa ya umeme.

Mzee huyo alimueleza Waziri Makamba kero yake hiyo wakati katika ziara ya kikazi ya Kijiji kwa Kijiji Wilayani Momba Mkoa wa songwe, eneo linalojengwa mradi mkubwa wa umeme wa TANZANIA NA ZAMBIA (TAZA).

“Sijawahi kuwasha kaswichi yani sijawahi,” alieleza mzee huyo.

Akijibu hoja ya mzee huyo, Waziri Makamba amesema, ” Mzee kama huyu jamani hajahawahi kuwasha taa ya umeme, sasa mzee tuombe Mungu umeme utawaka na utawasha taa.”

TAZA ni mradi mkubwa wa umeme unaotarajia kuondoa kero za hitaji hilo kwa Wananchi wa mikoa ya Rukwa na sehemu ya Katavi kutoka kununua umeme nchi Jirani ya Zambia.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments