Ticker

6/recent/ticker-posts

Chupa Limeamka na Chai..Bilnass na Nandy Wanatarajia Kupata Mtoto wao wa Kwanza

 


"Chupa limeamka na chai" hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya wanamuziki Billnass na Nandy ambao ni wachumba wa muda mrefu wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza pamoja.


Nandy kupitia ukurasa wake wa Instagram amethibitisha hilo kwa kupost picha ya ujauzito wake. "Asante Mungu kwa zawadi hii" - ameandika Nandy kwenye posti hiyo.


Wawili hao wanatarajia kufunga ndoa mwezi huu, huku sherehe yao ikitarajiwa kuwa ya aina yake.


Aidha, kwa mujibu wa Nandy wamekuwa kwenye mahusiano na Billnass tangu mwaka 2016, na Februari mwaka huu Nenga alimvisha Nandy pete ya uchumba

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments