Ticker

6/recent/ticker-posts

Uongozi wa Yanga Wafunguka Bei ya Kumuuza Kiungo Wao Mshambuliaji, Feisal Salum

Kiungo wa Yanga, Feisal Salum.
UONGOZI wa Yanga, umeweka wazi bei ya kumuuza kiungo wao mshambuliaji, Feisal Salum kuwa ni shilingi bilioni moja, hivyo kama kuna timu yoyote itafikia makubaliano ya fedha hiyo, wataisikiliza.

Fei Toto amekuwa moja kati ya wachezaji bora ndani ya Yanga tangu atue hapo, huku pia akiwa na mchango mkubwa katika kikosi cha Taifa Stars.

Akizungumza juu ya thamani ya mchezaji huyo, Msemaji wa Yanga, Haji Manara, alisema: “Thamani ya Feisal Salum inafikia shilingi bilioni moja, kama kuna timu itatoka popote pale iwe ndani au nje ya nchi inamuhitaji bila kutoa kiasi hicho cha fedha sidhani kama tutaweza kuwasikiliza au kukaa kwa mazungumzo yoyote.

“Feisal ni mchezaji mkubwa na ana mkataba na Yanga, sio kweli kwamba hakuna ofa ambazo zinakuja hapa nchini kwa ajili yake, zipo timu nyingi zimeonesha nia ya kumtaka, lakini ofa zake ni ndogo ndio maana hatutaki hata kuzisikiliza.”


 
Hivi karibuni, ilielezwa kwamba, Fei Toto anatakiwa na moja ya timu kutoka Ufaransa, lakini Yanga haikuwa tayari kumuachia.

STORI NA MARCO MZUMBE

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments