Ticker

6/recent/ticker-posts

Irene Uwoya Apigiwa Saluti Dubai Bata Anazokula ni Balaa, Afunguka Mazito


Irene Pancras Uwoya; ni staa mkali wa Bongo Movies ambaye amepigiwa saluti za kutosha na wakazi mbalimbali wa huko Dubai na hata baadhi ya Wabongo waishio humo kutokana na bata anazokula na sehemu mbalimbali anazotembelea.

Sehemu anazokula bata kipande hicho ni zile  ambazo hutembelewa na mastaa wa Dunia kama katika Dubai Mall na Burj Khalifa.

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA moja kwa moja kutoka Dubai, Uwoya anasema kuwa, anawashangaa wanaomshangaa anavyokula bata kwa maana hiyo ndiyo aina ya maisha yake ya kila siku.
Uwoya anaongeza kuwa, anafanya hivyo kwa ajili yake na afya ya akili yake kwani ni lazima apate muda mzuri wa kupumzika.

“Watu wengi unakuta wanajiuliza bata ninazokula, lakini watambue hata wao wanatakiwa kula bata kwa kadiri wawezavyo ili kuweka afya za akili zao katika hali nzuri na hata kutengeneza nafsi zenye furaha siku zote,” anasema Uwoya ambaye yuko nchini humo na mtoto wake na kampani yake.

Mara kwa mara, Uwoya amekuwa na safari nyingi za Dubai kwa ajili ya bata huku nyuma akiacha maswali kedekede juu ya ni wapi anapopata mamilioni ya pesa anayoteketeza kila kukicha.

Stori; Imelda Mtema, Dar

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments