Ticker

6/recent/ticker-posts

Kusah: Mwendo Nimeumaliza Kwa Aunty Ezekiel, Ukweli ni Nimeshikwa na NikashikikaStaa wa Bongo Fleva, Kusah.
Kusah; ni staa mwingine mkubwa wa Bongo Fleva ambaye anafunguka kuwa, kwa mahaba anayopewa na mzazi mwenzake, muigizaji Aunty Ezekiel, hakuna wa kumtoa hapo.

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Kusah anasema kuwa, anampenda Aunty leo, kesho na hata milele na kwamba mwendo ameumaliza kwa mama huyo wa watoto wawili.


Muigizaji Aunty Ezekiel
“Kwa kweli siwezi kuwa mnafki, ukweli ni kwamba nimeshikwa na nikashikika, hakuna wa kuweza kunichomoa kwa Aunty wangu, nampenda leo, kesho na hata milele. Kifupi kwake mwendo nimeumaliza,” anasema Kusah ambaye amejaaliwa mtoto wa kiume na Aunty waliyempa jina la Norma au Nono.

Stori; Khadija Bakari, Dar

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments