Ticker

6/recent/ticker-posts

Paula Masaja Atanua na Gari la Mama yake Aliyonunua Harmonize


PAULA Kajala au Pau; ni mrembo maarufu kwenye mitandao ya kijamii (sosholaiti) nchini Tanzania ambaye wikiendi iliyopita, Julai 15 ilikuwa ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake (birthday) ambapo siku hiyo ilipambwa na matukio mengi.

Ukiacha tukio la kuweka bango kubwa la birthday yake, pia Paula alionekana akitumia gari aina ya Range Rover la rangi nyeupe ambalo mama yake, Kajala Masanja amenunuliwa na mchumba’ke, Harmonize.

Kwa mujibu wa walimwengu, Paula anamchukia baba wa kambo, Harmonize baada ya kudai baba yake ni Majani pekee ila anatembelea Range Rover aliyonunuliwa mama’ke na baba huyohuyo wa kambo.

Mbali na hilo, pia watu wa karibu wanasema shughuli zote ikiwemo pati ya tukio hilo imegharamiwa na Harmonize.

Kitaalam walimwengu wanasema hiyo ni sawa na kusema; kitimoto sili ila mchuzi wake nakunywa…”

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments