Wafungwa kupata likizo ili kuzoeana na familia zao

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Wadau wa Mahakama mkoani Kigoma wameazimia kwa pamoja kuanza kutekeleza adhabu mbadala kwa wafungwa ikiwemo kutoa likizo kwa lengo la kuwawezesha wafungwa kuandaa maisha nje ya kifungo na kuishi karibu na familia zao wakiendelea kufanya kazi za maendeleo.
Adhabu mbadala kwa wafungwa ikiwemo kupewa likizo itahusisha wafungwa wenye vifungo chini ya miaka mitatu hatua itakayosaidia  kupunguza msongamano wa wafungwa gerezani.

Mkurugenzi Msaidizi idara ya huduma za uangalizi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Nsanze, amesema hatua hiyo itasaidia wafungwa kuzoeana na familia zao na kujiongezea kipato na kutoka vifungoni wakiwa tayari na mahusiano mazuri na familia.

Kwa upande wake Afisa Mhifadhi Wakimbizi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR mkoa wa Kigoma Rehema Msami, ambao wameratibu vikao vya kuwakutanisha wadau wa sheria mkoani Kigoma, wameomba pia wafungwa ambao ni wakimbizi kuwa sehemu ya mpango wa vifungo mbadala kulingana na sheria inavyoelekeza.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad