Abdu Kiba Afunguka "Ali Kiba Aliona Akitukanwa Akacheka tu, Watanzania Wanamjua Baraka The Prince"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Weekend iliyopita, Msanii wa Bongo Flava Barakah The Prince akiwa kwenye moja ya show na tungi nyingi kichwani huko jijini Mwanza, aliropoka kuwa hampendi @officialalikiba na ni Mpumbavu akitaka hadi mashabiki kuto hudhuria show za King, jambo ambalo liliamsha hasira za mashabiki wengi mitandaoni, si wa Alikiba tu bali wa muziki kiujumla wakimkosoa vikali msanii huyo. Na hii ilikuja baada ya mashabiki walio hudhuria show hiyo, kumtaka msanii huyo kuperform wimbo wake wa Nisamehe aliomshirikisha King Kiba.

Hasa kupitia Amplifaya ya Clouds Fm hii leo Sep 06, amesikika @officialabdukibaa akieleza kuwa Video clip hiyo ilimfikia kaka yake (Alikiba) akaishia kucheka tu, akiongezea kuwa tabia ya Baraka inajulikana na watanzania wengi. Kuhusu kumpokea Baraka kwa niaba ya kaka yake kama ataomba radhi na kutaka kujiunga Kings Music, Abdu amedai hawezi fanya hilo, kama amemkosea heshima mkubwa wake, hawezi kumbatia ujinga. Kingine Abdukiba amechukua sehemu ya maneno ya Chidi Benz kwenye moja ya interview aliyowahi kuifanya akisema “... Kama unaniona mimi chizi, jiulize mi nakuonaje...” na ndivyo Ali anavyo mtazama Baraka kwa kile alicho kiongea.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad