Kutangulia Sio Kufika...Diamond Platnumz Alianza Kuzikanyaga Kapeti za BET Kabla ya Burna Boy..Kilichotokea Sasa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Diamond Platnumz ndiye msanii wa kwanza tokea Afrika Mashariki na hata mbele ya Burna Boy, kuwa nominated kwenye tuzo za BET, ambapo kwa mara ya kwanza alikuwa nominated kwenye tuzo hizo mwaka 2014 katika kipengere cha “Best International Act” na bahati mbaya kwake ni kuwa hakufanikiwa kubeba tuzo hiyo mbela ya Davido aliyeinyakua. Ilimchukua mwaka mmoja tu kukaa kitaa kabla BET hawajamtaja tena Diamond kuwania kipengere hicho mwaka 2016, ikiwa ni mara yake ya pili, hakufanikiwa pia kuchukua tuzo hiyo mbele ya Black Coffee (Mshindi) tokea South Afrika. Miaka 5 mbele (2021), Diamond anakuwa nominated tena kwa mara ya 3,anaambulia patupu mbele ya Burna Boy (mshindi).


Waswahili wanakwambia kuchelewa sio kufika, wakati Diamond anakanyaga Red Carpet ya BET mwaka 2014, Burna Boy anafanya shows za Kidimbwi pale Lagos nchini Nigeria, Miaka mitano mbele (2019), Burna Boy anakuwa mkubwa ndani na nje ya bara la Afrika kupitia Album yake ya African Giant, hasa projects zilizo ibeba Album hiyo, On the Low na Gbona, anaingia kwenye tuzo za BET kwa mara ya kwanza na kuibeba tuzo hiyo kwenye kipengere cha Best International Act. Hakuishia hapo tu, akaibeba tena tuzo hiyo kwa miaka mingine miwili mbele mfululizo, 2020 na 2021 ambapo anakutana na Simba miaka 8 mbele kwenye tuzo hizo toka Diamond awe nominated kwa mara ya kwanza.


Kinacho wafananisha Diamond na Burna Boy kwenye BET, wote wamekuwa nominated mara 3, na kinacho watofautisha, Burna Boy kabeba tuzo hiyo kwenye nominations zake zote 3, wakati Diamond akikosa kwenye nominations zake zote 3.

19 h

See Translation

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad