Mkataba wMzungu wa Simba Awaaga Mashabiki Kupitia Instagram!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




MCHEZAJI wa Klabu ya Simba, Dejan Georgijevic almaarufu Mzungu, ametangaza kuvunjika kwa mkataba wake na klabu hiyo, huku akieleza kwa kifupi kwamba sababu kubwa ni kukiukwa kwa baadhi ya vipengele kwenye mkataba wake.

Kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram, Dejan ameandika:

“I confirm that my Contract of Employment is terminated with just cause due to the fundamental breaches of the Contract by the Club. Thank you fans for the support and love you have given me.”

(Nathibitisha kuvunjika kwa mkataba wangu wa ajira kwa sababu ya ukiukwaji wa mambo ya msingi katika mkataba wangu uliofanywa na klabu. Nawashukuru mashabiki kwa sapoti na mapenzi makubwa waliyonipa!)


Bado hakuna taarifa rasmi kutokea upande wa uongozi wa Klabu ya Simba kuhusu kuvunjika kwa mkataba huo.

Hatua hiyo, inakuja siku chache tangu Dejan alipoonekana akizozana na mchezaji mwenzake, Augustine Okra katika mechi ya kirafiki kati ya Simba na Malindi iliyochezwa visiwani Zanzibar.

Tangu kusajiliwa kwake mwanzoni mwa msimu huu, Dejan amefanikiwa kufunga bao moja pekee kwenye michezo ya Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Kagera Sugar na kwa muda mfupi alioihudumia timu hiyo, amekuwa gumzo kubwa miongoni mwa mashabiki wa soka nchini.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad