Mfanyakazi auawa kukataa penzi la mtoto wa bosi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mfanyakazi auawa kukataa penzi la mtoto wa bosi
Grace Wangoi, 32, kutoka Kapkoi mkabala na Moi's Bridge mjini Kitale, kaunti ya Trans Nzoia, alikuwa msaidizi wa mzee mmoja raia wa Canada kabla ya mwanawe anayeishi Canada kumtembelea nchini Misri.

Akizungumzia tukio hilo, Linda Shiundu, dada yake Wangoi, Tabby Wanja, ambaye anafanya kazi kama kijakazi nchini Saudi Arabia, alisema walipokea habari za kifo cha jamaa wao kutoka kwa rafiki.

“Nina dada yangu mmoja yuko Cairo, Misri, alikuwa anafanya kazi kwenye nyumba mpya, kulikuwa na mzee mmoja tu ndani ya nyumba hiyo kumtunza kulea basi mtoto wa yule mzee akaja kutoka Canada,” alisema Wanja.

“Alianza kumvizia dada yangu, na alipomkataa, akampiga na kitu butu kichwani dada yangu alianguka na kufariki dunia,” aliongeza Wanja.

Kulingana na Wanja, mwanamume huyo alipogundua kuwa alikuwa amemuua Wangoi, alijirusha kutoka orofa ya 13 na kufa papo hapo.

Taarifa kutoka kwa wakala aliyemtafutia Wangoi kazi hiyo ilisema kuwa alisikia kuhusu nafasi ya kumtunza mzee lakini mwenye afya njema kutoka kwa rafiki yake, na akafuzu kwa hilo.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 32, aliripoti kwenye nyumba hiyo Jumatano, Septemba 14, na muda mfupi baadaye, alilalamika kuhusu mwanawe bosi wake kwa wakala wake akisema alikuwa akimsumbua sana.

"Nilituma ujumbe kwa familia ya mzee huyo kuuliza ni nani mwingine alikuwa katika nyumba hiyo ilhali mlisema kulikuwa na mzee tu kwenye nyumba hiyo na ghafla kuna mtoto wa kiume ambaye sasa anamsumbua Grace," alisema,

Familia ya mzee huyo ilimjibu wakala huyo ikisema kijana huyo alikuwa anatarajiwa kuondoka baada ya siku chache na hivyo kumtaka Wangoi kuwa na subira kwani kila kitu kitakuwa sawa mara tu atakapoondoka.

Mwanamke huyo hakulalamika tena hadi Alhamisi jioni, alipomtumia wakala wake jumbe kadhaa na hata kujaribu kumpigia simu, lakini alikuwa amelala hivyo hakusikia simu yake ikiita.

Wakala huyo aliamka asubuhi na kupokea jumbe za kuzua hofu, na pia alipata ujumbe kutoka kwa mume wa Wangoi ambaye alilalamika kwamba hakuwa anapatikana kwenye simu yake.

Ajenti huyo pia alipokea ujumbe kutoka kwa dereva wake akisema kuwa familia ya mzee huyo ilikuwa ikiomba pasipoti ya Wangoi kwa sababu huenda alifariki.

Wakala huyo alishawishika mara moja kwamba Wangoi aliuawa kutokana na jumbe alizomtumia usiku.

"Nilipokea simu kutoka kwa polisi ikisema usiku ule, jamaa huyo alikuwa amempiga Wangoi na kitu kichwani na kujirusha kutoka ghorofa ya 13. Hivyo wote wawili wamekufa," alisema.



----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad