Miaka saba jela, faini Sh15 milioni kwa kumkashifu Rais Samia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Bariadi. Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Simiyu imemhukumu kifungo cha miaka saba na faini ya Sh15 milioni, Levinus Kidanabi maarufu kama 'Chief Son's kwa makosa matatu ikiwamo kumkashifu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Hukumu hiyo imetolewa leo Ijumaa Oktoba 21, 2022 na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Matha Mahumbuga ambapo alieleza kuwa mtuhumiwa alitoa taarifa za uongo kinyume cha Sheria ya Makosa ya Kimtandao ya Mwaka 2015.

Katika taarifa iliyotolewa Wakili wa Serikali Daniel Masambu imeeleza kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa anashtakiwa kwa kosa la kuchapisha taarifa za uongo katika Jukwaa la Mtandao wa Whatsapp la "Simiyu Breaking News".

Ameeleza kuwa shtaka la kwanza na la pili alitenda Desemba 03 na 04, 2021 mtuhumiwa huyo aliandika kwenye jukwaa hilo maneno ya kumkashifu Rais Samia Suluhu Hassan.

Shtaka la tatu ni kutumia namba ya simu  0764996612  isivyo kihalali iliyokuwa imesajiliwa kwa jina la Hollo Yonas bila kuwa na kibaki kutoka mamlaka husika.

"Katika makosa hayo yote mshtakiwa amehukumiwa kutumia kifungu cha miaka mitatu jela na faini ya Sh5 milioni kwa kosa la kwanza, miaka miwili jela na faini ya Sh5 milioni kwa kosa la pili na miaka miwili jela pamoja na faini ya Sh5 milioni kwa kosa la tatu," amesema Masambu.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad