Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Nchini Harmonize, Zuchu Wateka Kijiji Kimyakimya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Harmonize au Konde Boy na Zuchu; ni wasanii wa muziki wa Kizazi Kipya nchini Tanzania ambao wameteka Kijiji cha Mtandao wa YouTube ambapo nyimbo zao zinashika nafasi za juu kabisa zikijizolea mamilioni ya wasikilizaji na watazamani (views).

 

Katika nyimbo tano za juu kabisa kuanzia namba moja hadi namba tano; nyimbo tatu ni za Harmonize na mbili ni za Zuchu.

Harmonize au Harmo anashika namba moja na wimbo wake wa Nitaubeba ukiwa umejikusanyia views zaidi ya milioni 4.5.

 

Lakini nyuma yake anakimbizwa kimyakimya na Zuchu akiwa na wimbo wake wa Kwikwi ambao unashika namba mbili ukiwa umejikusanyia views zaidi ya milioni 1.


Mwanamuziki nyota wa WCB, Zuhura Othman Soud anayefahamika zaidi kwa jina la kisanii ‘Zuchu’.

Namba tatu ya YouTube Trending Music inarudi kwa Harmonize na wimbo wake mwingine wa Amelowa ambao umejikusanyia views zaidi ya milioni 2.7.

 

Zuchu anaonekana tena kwenye namba nne na wimbo wake wa Love akiwa amemshirikisha msanii wa Nigeria, Adenkule Gold ambao una zaidi ya views milioni 1.1.

 

Namba tano inashikiliwa tena na Harmonize na wimbo wake wa Leave Me Alone akiwa amemshirikisha Abigail Chams ambao una views zaidi ya laki 5.

STORI NA SIFAEL PAUL | GPL


----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad