Japo Wanadiss ila Harmonize Kafikisha Lengo, Kuwataja Kipara na Asake wa Tandale Ngoma Itaenda

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Kitu kimoja ambacho @harmonize_tz anakifaulu zaidi kwenye muziki wake ni kutosikiliza kelele za mitandaoni na kutokuwa muoga nazo, kwasababu game ni imbalance, tunapenda kunyooshea watu vidole wale tusio wapenda kuwa wanakosea, hata kama yule unayempenda anakosea pia. Naona reactions za watu wengi ni juu ya Verse ya Harmonize kwenye wimbo wa Kontawa, #champion hasa kuhusu kutaja majina ya baadhi ya watu.

Harmonize ametaja watu kama Anjella, Killy na Cheed kuwa haikuwa riziki kwa Konde Gang, lakini Pia kawataja Diamond kama Asake wa Tandale na Sallam Sk kama Kipara. Turudi kwenye point, hawa wote wametajwa kama sehemu ya watu waliokuwemo kwenye safari ya Harmonize hadi kufikia uchampion wake, yeye ndiye anaye jua picha ya ndani zaidi ya kile tunacho kijua sisi.

Majungu ni nini? Na Sanaa ni nini? Binafsi sio muumini wa muziki uliojaa majina lakini kwanini tuiponde Champion Remix na kuona Harmonize kakosea wakati tuliipa kitiki cha Blue Fresh Remix? Au kisa wametajwa Diamond na Sallam? Kama Verse ya Harmonize kwenye Champion ni majungu, Verse ya Diamond ni nini kwenye Fresh Remix? Hadi mashabiki wa Alikiba wakafanya Ngosha akonde, Hivi kuna msanii kawataja vibaya maEX wake kwenye nyimbo zake tena kwa majina kama Diamond? Ref. #Katika ya #navykenzo , Kwanini Harmonize?

Kwa kifupi malengo ya Remix yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa, maana ndicho kinacho trend mitandaoni hivi sasa, iwe kwa ubaya ama uzuri. Na ni muda wa Kontawa kuonyesha kuwa yeye ni msanii wa wote bila kujali atashirikiana na nani, kikubwa kazi ifike mjini.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad