Mapacha Waliozaliwa Kwa Ujauzito Wa Miezi 4 Wavunja Rekodi Ya Guinness

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Watoto Adiah na Adrial Nadarajah wameweka rekodi mpya na kupita rekodi ya awali ya Siku 125 iliyowekwa Mwaka 2018 na Mapacha wengine kutoka Jimbo la Iowa, Marekani


Kwa mujibu wa Guinness, Watoto hao wamezaliwa zikiwa zimesalia Wiki 18 kufika Wiki 40 zinazotakiwa Kiafya kwa Mama Mjamzito ili Mtoto akue vizuri


Mama wa Mapacha alijifungua katika Wiki ya 21 na Saa 22 huku Madaktari wakimwambia Watoto wake wana 0% ya kuishi. Adiah na Adrial wamefikisha Mwaka mmoja, licha ya matatizo makubwa ya Kiafya waliyopitia.


Ilikuwa mimba yake ya pili, baada ya kupoteza mimba yake ya kwanza miezi michache iliyopita katika hospitali hiyo hiyo karibu na nyumbani kwao huko Ontario.




Muda ambao mimba inakuwa iko tayari kawaida ni wiki 40, na hilo lilifanya watoto hao kuzaliwa kabla ya wakati kwa wiki 18.


Baba Kevin Nadarajah alisema kuwa hospitali iliwaambia hawataweza kusaidia na ujauzito huo ambao watoto walizaliwa mapema zaidi, na kumwacha macho usiku kucha akisali na “uso ukibubujikwa na machozi”.


Hospitali nyingi hazijaribu kuokoa maisha ya watoto waliozaliwa kabla ya wiki 24 hadi 26.


Lakini kwa bahati nzuri, wanandoa hao waliweza kuhamia Hospitali ya Mount Sinai huko Toronto, ambayo ina kitengo maalum cha uangalizi wa watoto wachanga.


Katika siku ya pili ya uchungu wa Bibi Rajendram – wiki 21 na siku sita za ujauzito – aliambiwa kwamba ikiwa watoto wangezaliwa hata dakika chache kabla ya wiki 22, wangefariki.


Licha ya kutokwa na damu nyingi, alisema alijaribu kila awezalo kuwazuia watoto ndani ya tumbo kwa saa chache zaidi.


Maji yake hatimaye yalikatika dakika 15 baada ya saa sita usiku. Chini ya saa mbili tu baada ya kuingia wiki 22 tumboni, watoto walizaliwa.


Adiah na Adrial sasa wameishi hadi kufikisha umri wa mwaka mmoja, licha ya matatizo makubwa ya kiafya wakati wa awali.


“Tulitazama watoto karibu kufa mbele ya macho yetu mara nyingi,” Bi Rajendram alisema. Wakati bado wanafuatiliwa kwa karibu na madaktari, ndugu hawa “wanaendelea vizuri”.


Mtoto aliyezaliwa kabla ya wakati zaidi alikuwa Curtis Means wa Alabama, ambaye alizaliwa akiwa na wiki 21 na siku moja.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad