Yanga "Kocha Nabi Aondoke? Mnaumwa Nyie!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



YANGA juzi usiku ilikuwa uwanjani ikisaka heshima yake ya kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, lakini nyuma mabosi wao wakafunga mjadala wa hatma ya kocha mkuu wa timu hiyo, Nasreddine Nabi wakisema jamaa bado yupo sana klabuni.

Timu hiyo iliyopo Kundi D sambamba na Monastir ya Tunisia, Real Bamako ya Mali na TP Mazembe ya DR Congo na akizungumza na Mwanaspoti, Makamu wa Rais wa Yanga Arafata Haji amefunga mjadala akisema wanajua thamani ya makocha wote walionao na sio Nabi pekee.

Arafat alisema, tayari Nabi anafahamu kuwa mkataba wa kusalia Yanga zaidi uko mezani kwake ni suala la kuamua tu lini asaini kwa kuwa uongozi wao tayari ulishampa uamuzi wao wa kutaka kumbakiza zaidi.

Alisema bado wana malengo makubwa katika kuunda timu bora na kwamba kitu pekee ambacho kinawatofautisha na wapinzani wao wengi ni kuwa na benchi la ufundi pana lenye wataalam bora.

"Nabi kuondoka linawezekana lakini haiwezi kuwa sasa, nadhani hata yeye anaamini yuko katika klabu ambayo hatua chache zijazo anaweza kuwa katika rekodi kubwa zaidi ya mafanikio," alisema Arafat na kuongeza;

"Bado tunamhitaji sana Nabi niwahakikishie mashabiki wetu kwamba kocha wao huyu na mwingine haitakuwa rahisi kwetu kuwaachia, tuna malengo makubwa na hii ni safari tu ya kufika huko. Tunafahamu hizi taarifa za sisi kuwa na kocha bora kama Nabi wengine ni ndoto zao, Yanga tuko katika mafanikio haya kutokana na kutumia nguvu kuwaweka wataalam wote bora kama hawa, utulivu wa namna hii klabu zingine hazina ndio maana wanayumba kila wakati."
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad