Beyonce Aandika Historia, Afanya Shoo baab'kubwa

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa

 

Beyonce Aandika Historia, Afanya Shoo baab'kubwa

Mashabiki wapatao 60,000 wa Beyoncé walimiminika Cardiff kushuhudia onyesho la uzunduzi wa safari yake ya muziki wake katika maeneo mbalimbali ya dunia.


Watu walisafiri kutoka maeneo mbalimbali duniani kumuona muimbaji huyo akiwa jukwani katika Uwanja wa Principality.


Walitoka maeneo ya mbali kama vile Marekani, Lebanon na Australia na walikuwa wameanza kupanga misururu saa 12 kabla ya onyesho kuanza Jumatano.


Mmoja wa mashabiki alisema anamkubali sana Beyonce na hata angefurahi "iwapo angenipaka jasho lake".


Watu walisafiri kutoka kote duniani kumuona mwanamuziki kwenye jukwaa la Principality Stadium


George Crocker, 15, ambaye alikuja kutoka Avoca Beach, New South Wales, Australia, alisema: "Ninashukuru sana kwamba fursa hii imekuja, kwamba hatimaye ninaweza kumuona.


"Ni mungu wa kike, ni mama yangu. Ni malkia kabisa…ni kila kitu katika mtu. Kila kitu kumuhusu ni kamili."


Shabiki wa Beyonce tangu akiwa na umri wa miaka minne, alisafiri na mama yake Penny, na kuongeza: "Nitakuwa nimekodoa macho yang utu wakati wote , ninafahamu hilo kusema kweli."


Giovani Tana, 20, aliwasili katika mji mkuu wa Wales Jumamosi, baada ya kusafiri kwa ndege hadi London kutoka Beirut, Lebanon, na kupanda treni.


"Ni mara yangu ya kwanza kufika Uingereza, kwahiyo ni sababu kuu ya kuja," alisema.


"Nadhani London inafahamika zaidi na nilifikiria kuufahamu mji tofauti’’


"Kazi yake ni nzuri sana. Hakuna anayeweza kufanya ‘’shoo’’ kama anavyoifanya’’


"Ninaiheshimu kazi yake na kile anachokifanya kwa jamii ya wapenzi wa jinsia moja ni ya kufurahisha’’


"Kwake kuwa jukwaani kunawakilisha matamanio ya watu tofauti."


Madada Emma na Stephanie Dalton walisafiri kutoka Dublin kwa ajili ya tamasha na walikuwa katika msururuwa kuingia uwanjani mapema Jumatano


Emma, 28, alisema: "Tuna furaha kubwa, kwahiyo kuja mapema ni bora zaidi.’’


Tamasha la Renaissance World Tour ni la kwanza kufanywa na Beyoncé mwenye umri wa miaka 41-year-katika kipindi cha miaka saba.

_________

LOVE STORY YA UTANIKUMBUKA NEYLA Ipo tayari ni maandishi na Sauti !, Kuisoma yote Bonyeza HAPA Lipia tsh 1000 Tu mtandao wowote,au Tembelea www.makapedia.com

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad