Ngoma Bado Ngumu Kariakoo, Wafanyabiashara Wagoma Kufungua Maduka

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Dar es Salaam. Licha ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla kumaliza mgomo wa wafanyabiashara na kuwataka warejee katika biashara zao, ngoma bado ngumu kwa Mwenyekiti wa soko hilo baada ya wafanyabiashara kugoma kufungua biashara.

Hiyo ni kutokana na kile walichoeleza kuwa wako tayari kufunga maduka hadi jioni kama hawatasikilizwa huku wakimtaka Rais kuwasikiliza.

Msimamo huo walianza kuuonyesha tangu Makalla akizungumza kwani katika baadhi ya vitu alivyosema wafanyabiashara walikuwa wakitoa sauti za kugomea kile anachokizungumza hasa aliposema kuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa atafanya kikao na kamati ya wafanyabiashara wa soko hilo siku ya Alhamisi Dodoma.

Wafanyabiashara walisema hawaoni sababu ya wao kumfuata Waziri Mkuu Dodoma badala ya wao kufuatwa Kariakoo.


Licha ya kuonyesha kukubali lakini wafanyabiashara walibaki katika eneo hilo jambo lililomfanya mwenyekiti kuanza kuzungumza nao huku akiwasisitiza warejee katika biashara zao.

Mmoja wa wafanyabiadhara ambaye hakutaja jina lake alipopewa nafasi ya kuzungumza ikiwa wanataka kurejea katika biashara alisema lengo lao lilikuwa kukutana na Rais Samia Suluhu Hassan na si Mkuu wa Mkoa.

"Hawa wote waliokuja tumeshawasikiliza, Waziri wa Fedha ameshatusikiliza na hakuna kilichofanyika," alisema mfanyabiashara huyo huku akishangiliwa na wafanyabiashara wenzake.

Honest Kalisti Mjunbe wa Jumuiya ya wafanyabiashara amesema hakuna kurudi nyuma katika hili waliloanzisha

"Mambo ya siasa kwenye biashara zetu hatuhitaji siasa hazina nafasi, Waziri mkuu si kama hajui, Mwigulu Nchemba si Kama hajui, Mkuu wa Mkoa na Wilaya wanajua lakini hakuna kilichofanyika,"amesema.

"Cha msingi waende wakae kwenye kamati yao sisi maduka tunafunga ili tuonane na Rais Samia Suluhu Hassan,”ameongeza.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad