Polisi yafafanua tukio aliyekufa kwa kujirusha toka Ghorofani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Polisi yafafanua tukio aliyekufa kwa kujirusha toka Ghorofani


Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa, imesema mifumo ya kamera imeonesha Joel Misesemo alijirusha toka ghorofani kwa makusudi kupitia dirisha lililopo ghorofa ya saba.


Kauli ya Mambosasa inakuja kufuatia tukio la Mei 23, 2023 la mtu huyo mkazi wa Mwananyamala ambaye alikuwa ni mshereheshahi ‘MC’ na anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 35 na 40, kujirusha kutoka ghorofa ya saba katika jengo la Derm Plaza lililopo Makumbusho na kufariki.


Taarifa hiyo imeeleza kuwa, “uchunguzi wa awali unaonesha marehemu alionekana katika jengo hilo tarehe 23, Mei 2023 majira ya saa 11:40 alifajiri na alimwambia mlinzi wa zamu kuwa anaenda kufanya ibada kwenye msikiti uliopo ghorofa ya 15 ndani ya jengo hilo, hata hivyo muda mfupi baadaye alijirusha kutoka juu ghorofani na kuanguka chini.”


Aidha, tarifa hiyo pia inaeleza kwamba, “mifumo ya kamera ya jengo hilo inamuonesha mtu huyo akijirusha kwa makusudi kutoka ghorofa ya saba kupitia dirishani, mwili wake umepelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala kwa uchunguzi zaidi.”

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad