Simba Yagomea Ofa Ya Onyango.. Adaiwa Kuandika Barua Ya Kuomba Kuondoka

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Simba Yagomea Ofa Ya Onyango.. Adaiwa Kuandika Barua Ya Kuomba Kuondoka


UONGOZI wa Simba, umegomea ofa kutoka Klabu ya Gor Mahia ya nchini Kenya ambayo imeonesha nia ya kumuhitaji beki wa timu hiyo, Joash Onyango.


Hiyo ikiwa ni siku chache tangu tetesi zizagae za beki huyo raia wa Kenya, kuandika barua ya kuomba kuondoka Simba mwishoni mwa msimu huu.


Taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, Gor Mahia inayoshiriki Ligi Kuu ya Kenya, imewasilisha ofa hiyo, hivi karibuni ikiomba huduma ya beki huyo kwa ajili ya msimu ujao.


Mtoa taarifa huyo alisema, ofa hiyo imekataliwa na mabosi wa Simba, wakidai ni ndogo, huku wakiitaka Gor Mahia iongeze fedha ili wakamilishe dili hilo.


Aliongeza kuwa, Simba wapo tayari kumuachia beki huyo, kama makubaliano yatafikia sehemu nzuri kwani tayari wapo katika mazungumzo na mabeki waliopanga kuwasajili.


“Gor Mahia ya nchini Kenya imeonesha nia ya kutaka kumsajili Onyango kwa ajili ya msimu ujao, lakini Simba imegoma ikitaka iongezewe pesa na sio hiyo ofa ndogo waliowekewa mezani.


“Simba ipo tayari kumuachia Onyango kuondoka ila kwa timu itakayofika dau wanalolihitaji kama uongozi utafikia makubaliano mazuri.


“Bado mazungumzo yanaendelea kati ya uongozi wa Gor Mahia na Simba, kama makubaliano yakifikia pazuri, basi beki huyo hatakuwa sehemu ya wachezaji wetu msimu ujao,” alisema mtoa taarifa huyo.


Akizungumzia hilo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema kuwa: “Uongozi hivi sasa unafanya vikao pamoja na kocha Robertinho (Roberto Oliviera) kwa ajili kuweka mikakati ya usajili, kikubwa tumepanga kufanya usajili mkubwa utakaoendana na Simba ambao utatufikisha Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.”


STORI NA WILBERT MOLANDI

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad