Diamond Platnumz Aangukia Pua Tena Tuzo za BET

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Diamond Platnumz Aangukia Pua Tena Tuzo za BET

Msanii wa Bongofleva toka WCB Wasafi, Diamond Platnumz, kwa mara nyingine tena ametoswa kwenye tuzo za BET ukiwa ni mwaka wa pili mfululizo!.


Tuzo hizi zinaandaliwa na Black Entertainment Television (BET) toka Juni 19, 2001 zinalenga kusheherekea mafanikio ya kazi za Wamarekani Weusi katika sanaa ya muziki, uigizaji na michezo.


Ikumbukwe Diamond ndiye msanii wa kwanza Bongo kuchaguliwa kuwania tuzo za BET katika kipengele Best International Act, tayari amewania mara tatu (2014, 2016 & 2021) na kumfanya kuwa msanii pekee aliyewania mara nyingi.


Hata hivyo, katika orodha ya majina yaliyotoka hapo jana, jina la Diamond halipo licha ya mwaka uliopita kufanya vizuri na EP yake, First of All (FOA) iliyotoka Machi 2022 ikiwa na nyimbo 10.


Katika kipengele cha Best International Act ambacho Diamond amekuwa akiwania miaka yote, kuna Burna Boy, Ayra Starr (Nigeria), KO (Afrika Kusini) n.k.


Tuzo hizo zinazotarajiwa kutolewa Juni 25, 2023 katika ukumbi wa Microsoft Theater Jijini Los Angeles, Marekani.


Ikumbukwe Eddy Kenzo toka Uganda ndiye msanii wa kwanza Afrika Mashariki kushinda tuzo ya BET, mwaka 2015 aliibuka mshindi katika kipengele cha Viewer’s Choice Best New International Act, huku Rayvanny akishikilia rekodi upande wa Tanzania ambapo mwaka 2017 alishinda katika kipengele hicho pia.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad