Ghetto Kids ya Uganda yatinga fainali ya "Britain's got talent" 2023 - VIDEO

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Ghetto Kids ya Uganda yatinga fainali ya "Britain's got talent" 2023 - VIDEO


Watoto wanaocheza densi nchini Uganda kwa jina la ‘Ghetto Kids’ wamefanikiwa kutinga fainali ya shindano maarufu la uhalisia la vipaji, Britain's Got Talent.


Ghetto Kids walishangiliwa kwa namna yake na waliofika kutazama mashindano hayo moja kwa moja pamoja na majaji wote wanne kwa onyesho lao la kusisimua lililoonyeshwa Jumatano usiku.


Kufuatia maonyesho hayo, waandaji Ant na Dec walizungumza na majaji na Alesha Dixon na Simon Cowell wakachagua Ghetto Kids kama mchezo wao bora.


Watoto hao sita wenye umri wa miaka mitano hadi 13 ni yatima wanaoishi pamoja nchini Uganda baada ya kuasiliwa na baba yao Daouda Kavuma.


Sita hao ni miongoni mwa 31 ambao Daouda amewapa makao baada ya kuwapata wakiishi kwenye mitaa hatari ya jiji.


Wanatumia densi kuonyesha uwezo wao na kutimiza ndoto zao maishani.


Fainali ya mashindano ya Britain ya Got Talent itafanyika Jumapili, 4 Juni.

TAZAMA VIDEO:
_________

LOVE STORY YA UTANIKUMBUKA NEYLA Ipo tayari ni maandishi na Sauti !, Kuisoma yote Bonyeza HAPA Lipia tsh 1000 Tu mtandao wowote,au Tembelea www.makapedia.com

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad