Kuhusu Simba Kumsajili Winga Machachari wa ASEC Mimosas..Ishu Nzima Ipo Hivi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Kuhusu Simba Kumsajili Winga Machachari wa ASEC Mimosas..Ishu Nzima Ipo Hivi

Klabu ya Simba ipo sokoni kuangalia silaha za kuondoa aibu kwa msimu ujao na unyonge wa mashabiki wanaoupitia kwa msimu huu, ikidondosha mataji yote, tayari imetua nchini Ivory Coast ikiwinda winga la ASEC Mimosas, huku mastaa wakilimwa barua.

Winga ambaye Simba ipo naye kwenye mazungumzo mazito kuhakikisha inaipata saini yake kuja kuongeza nguvu zaidi kikosini anatajwa kwa jina la Kramo Aubin.

Huyo jamaa ni hatari kwa mikimbio na Simba ilishaonja joto la jiwe la mchezaji huyo aliwahi kuwafunga mwaka 2022 walipocheza Kombe la Shirikisho la Afrika, wakichapwa mabao 3-0 ugenini lakini pia msimu huu amekuwa bora kwenye michezo yote.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Simba kilisema kuwa uongozi upo kwenye hatua nzuri za mazungumzo kwa ajili ya kumalizana na staa huyo wa Asec ambaye wanaamini ataweza kuongeza kitu ndani ya timu.

“Mazungumzo na winga huyo ambaye ni mchezaji tegemeo wa kikosi cha ASEC Mimosas yanakwenda vizuri na kuhusu mchezaji mzawa tumemwambia kocha amfuatilie Shiza Kichuya kwasababu ni winga ambaye anasifa kama alizozitaja.

“Hivyo tunamsikilizia kama mambo yatakwenda kama ilivyopangwa tutaweza kufanya naye mazungumzo,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kimesema kuwa wanaendelea na usajili ili kukiandaa kikosi chao mapema kama mapendekezo ya kocha wao alivyotaka kuona wanasajili mapema ili kuingia kambini mapema kujiandaa na msimu mpya.

Kramo Aubin amecheza mechi nane za Kombe la Shirikisho Afrika na kuifungia timu yake mabao manne kwenye michezo hiyo moja alilifunga uwanja wa nyumbani na matatu kwenye michezo ya ugenini.

Staa huyo amecheza timu tatu tu hadi sasa zote zikiwa za nchini kwao Ivory Coast amekuzwa na ASEC Mimosas ambayo alianza kuitumikia mwaka 2015 akicheza kwa misimu miwili baadae akatimkia Africa Sports alicheza msimu mmoja, 2019 alitimkia FC San Penro na 2021 akaamua kurudi tena ASEC Mimosas ambayo anaitumikia hadi sasa.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad