Mayele na Saido Wapewa Tuzo ya Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara 2022/2023

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mayele na Saido Wapewa Tuzo ya Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara 2022/2023


Fiston Mayele wa Yanga na Saido Ntibazonkiza kutoka Simba wote wamepewa tuzo ya mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara 2022/23.

Mayele na Saido kila mmoja alifunga mabao 17 hivyo Kamati ya Tuzo ilikaa na kuangalia kanuni zinaelekezaje wachezaji wanapofunga mabao hivyo kila mmoja kupata tuzo.

Mayele ambaye ameenda kwenye majukumu ya timu yake ya Taifa DR Congo tuzo yake ilipokelewa na mke wake ambaye aliwashukuru kwa tuzo hiyo.

Hata hivyo Mayele amezungumza akiwa kwenye kambi ya timu ya Taifa akisema; "Nashukuru wote kuanzia viongozi, wachezaji, mashabiki walionipa sapoti kubwa.

"Hata mechi ya mwisho nililazikika kucheza huku nikipewa sapoti kubwa sana, natamani ningekuwepo ila nipo kwenye majukumu ya timu ya Taifa," amesema Mayele

Saido pia amewashukuru uongozi wa Geita Gold na Simba SC kumsaidia kubeba kiatu hicho

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad