Zari Adaiwa Kuwablock Mashabiki Kisa Kifaa Kipya cha Diamond Platnumz

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Tangu kuibuka kwa tetesi kuwa yuko kwenye mahusiano na staa wa bongo Diamond Platnumz, Watanzania wamekita kambi kwenye ukurasa wa mwimbaji wa dancehall wa Ghana, Francine Koffie almaarufu Fantana.

Mashabiki wengi Watanzania kwenye Instagram wamekuwa wakitoa maoni mseto kwenye kila post anazoweka mtandaoni huo, baadhi wakitoa maoni mazuri na kumsifia huku wengine wakimshambulia na kumsema vibaya.

Baadhi yao ambao wameonekana kuamini kabisa kuwa anachumbiana na bosi huyo wa WCB pia wamekuwa wakimvuta mzazi mwenzake, Zari Hassan kwenye mjadala. Baadhi wamemlalamikia Zari huku wengine wakimtetea.

Baadhi ya wanaomshabikia Fantana wameibua madai kwamba Zari amewablock baada ya kumzungumzia kwenye ukurasa wake.


"Wifi Zari kaniblock jamani," mwanamtandao mmoja aliandika kwenye chapisho la hivi punde la mwimbaji huyo wa dancehall.


Mwingine alisema, "Zari aliniblock kwa sababu nilicomment (Fantana) siku chache kabla ya premier ..wakati sikujua nini kilitokea kwenye shoo WOW. Inawezekanaje?"

Kundi la wanamitandao waliotoa maoni walionekana kumtambua mrembo huyo mwenye umri wa miaka 25 kama mpenziwe Diamond.

"Diamond Platnumz njoo umuone mke wako mpya, ni mrembo kupindukia," jaydon.tz alisema.

Mwingine alisema, "Fantana, anayemnyima Zari usingizi."

Hata hivyo, kuna baadhi ya wanamitandao ambao waliegemea upande wa Zari ambaye ana watoto wawili na Diamond.

"Zari ni mzuri zaidi na ana miguu mizuri," Sharon Masiga alisema.

Tetesi kuwa mwimbaji huyo wa Ghana anachumbiana na Diamond Platnumz ziliibuka baada ya kupeperushwa kwa sehemu ya pili ya Young, Famous and African.

Katika moja ya matukio kwenye filamu hiyo ya uhalisia, Diamond alionekana akibusiana kimahaba na Fantana.

“Nilijiona mimi ndiye bora kwa kubusu, hadi nilipombusu Fantana,” Diamond alisema kuhusu tukio hilo la kubusiana.

Alibainisha kuwa busu la Fantana lilikuwa zaidi ya busu.

"Hakuwa ananibusu, alikuwa akinila!" alisema.

Diamond aliweka wazi kuwa busu la malkia huyo wa Ghana lilikuwa bora zaidi kuwahi kupokea katika miaka yote 32 ya kuwepo kwake.

Aidha,Fantana alifichua kuwa Diamond alimwambia kuwa Zari alitaka mtoto mwingine naye, jambo lililozua mzozo baina ya wote watatu. Zari alimshtumu Diamond kwa kumtumia kuwateka wasichana na akamfuta katika maisha yake.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad