Kijana Amuua Mpenzi wa Mama yake Baada ya Kumkuta Chumbani na Mama

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa

Jeshi la Polisi Mkoani Arusha linamshikilia Kijana anayefahamika kwa jina la Rasuli Abdalah kwa tuhuma za kumuua Mwanaume anayefahamika kwa jina la Aniskari Maembe (pichani) baaada ya kumkuta akiwa amelala na Mama yake mzazi.

Noris Kivuyo ambaye ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Makao mapya ambako tukio limetokea amesema Mtoto huyo alimkuta Mama nyumbani kwa Mwanaume huyo na kumtaka atoke nje na alipogoma alimtoa kwa hasira akiwa uchi na baadaye akanza kumshambulia Mwanaume kwa marungu hadi kufariki.

“Nilipouliza nikaambiwa ni Mtoto amekuja kumtoa Mama yake kwenye chumba ndani kwa Mwanaume, Mama alivyogoma alimtoa akiwa uchi na Mama alipiga kelele sana, nitoe ushauri ukiona Baba yako anatoka na taulo kwenye chumba cha Mama yako huyo ni Baba yako”

Mwanamke huyo alishaachana na Mumewe na akawa kwenye mahusiano na Mwanaume aliyeuawa, bado hajajulikana chanzo cha Mtoto kuchukua maamuzi hayo.
_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad