Ajali Nyingine Mbaya Morogoro: Yauwa na Kajeruhi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Ajali Nyingine Mbaya Morogoro: Yauwa na Kajeruhi

Mto mmoja amefariki na wengine sita kujeruhiwa katika ajali iliyotokea usiku wa kuamkia Septemba 4, 2023 katika eneo la Mataa ya Tumbaku lililopo Manispaa ya Morogoro Barabara kuu ya Morogoro kuelekea Iringa.


Ajali hiyo, imehusisha Lori la mizigo lenye namba za usajili T 862 DNH lililokua linatokea Dar es Salaam Kuelekea Iringa, kugongana na Basi la Abiria aina ya Tata, lenye namba za usajili T 994 DCH lililokua linatokea kituo cha Mabasi Mafiga Kuelekea Msamvu.


Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Mkoani Morogoro amesema baada ya kufika katika tukio walifanya maokozi huku Majeruhi wakiwapatia huduma ya kwanza kabla ya kukimbizwa Hospitali na kwamba aliyefariki kwenye ajali hiyo ni Dereva wa Lori hilo na waliojeruhiwa ni abiria watano na dereva waliokuwepo kwenye basi la abiria.


Mashuhuda wa ajali hiyo wanasema walisikia mlio mkubwa mara tatu na waliposongelea eneo la tukio walikuta Dereva wa Lori amebanwa huku akivuja damu na wasafiri waliokuwa kwenye basi la abiria wakiwa na majeraha, huku chanzo cha ajali hiyo kikitajwa kuwa ni uzembe wa dereva wa Lori ambaye ni marehemu kuendesha kwa mwendokasi
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad