Tajiri wa Tumbaku Shinyanga Adaiwa Kujiua kwa risasi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





Kahama. Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Ulowa ambaye ni mfanyabiashara na mkulima maarufu wa tumbaku, Safari Manjala anadaiwa kujiua kwa kujipiga risasi chini ya kidevu.

Inadaiwa Manjala alijiua jana saa mbili asubuhi baada ya kuamka na kwenda kwenye shamba lake la miti katika Kijiji cha Ilomelo kilichopo Halmashauri ya Ushetu, wilayani Kahama.

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Wilaya ya Kahama, Hassan Ramadhan akizungumzia tukio hilo alisema limewashtua.

“Kweli tumepata taarifa za msiba wa mwanachama wetu, taarifa tulizopata kutoka kwenye familia yake ni kwamba aliamka asubuhi akaenda shambani kwake na baada ya muda walisikia mlio wa risasi na kukuta amejiua,” alisema.

Alisema chama hicho kinaendelea na taratibu zingine kikisubiri taarifa ya Jeshi la Polisi kujua chanzo cha tukio hilo.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Kennedy Mgani amethibitisha tukio hilo na kueleza kuwa anasubiri taarifa kutoka kwa wasaidizi wake.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad