Kocha Gamondi Achekelea Kupata Tuzo ya Kocha BORA "Hii ni Tuzo Yenu Wananchi"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Kocha Gamondi Achekelea Kupata Tuzo ya Kocha BORA "Hii ni Tuzo Yenu Wananchi"

 Kocha Gamondi Achekelea Kupata Tuzo ya Kocha BORA "Hii ni Tuzo Yenu Wananchi"

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amechekelea hatua ya kupata tuzo yake ya kwanza nchini akiwa kocha bora wa mwezi huku akiitoa kwa mashabiki wa timu hiyo.


Kupitia taarifa iliyotolewa jana na Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) Gamondi ametajwa kuwa kocha bora wa mwezi Agosti akiwashinda wenzake Roberto Oliveira 'Robertinho' wa Simba na Hemed Morocco wa Geita Gold.


Gamondi amesema tuzo hiyo ni Zawadi kwa mashabiki wao ambao wakati wote wamekuwa karibu yao bila kujali matokeo ambayo wanayapata uwanjani.


Kocha huyo raia wa Argentina pia ametumia tuzo hiyo kuwapongeza wachezaji wake akiwatambua kuwa ndio watu muhimu kwenye kazi yake kwa kupigania ushindi wa timu hiyo.


"Ni furaha kubwa kupata zawadi ya namna hii, kwangu Mimi hii ni zawadi kwa mashabiki wetu, siku zote wako nasi bila kujali matokeo ambayo tunayapata uwanjani, tunajituma kazini ili wao wafurahi,"amesema Gamondi ambaye kwenye mechi mbili za ligi ameiwezesha Yanga kushinda alama zote 6 na mabao 10.


"Wachezaji wetu nao wanamchango wao mkubwa kwenye hili, unajua sisi makocha sio kitu kama hakuna wachezaji Bora kama hawa tulionao ambao ndio wanafanya kazi kubwa uwanjani kwa kujituma kwao.


"Tuzo ya namna hii ni matokeo ya umoja na kufanya kazi kwa ushirikiano kuanzia watu wanaofanya kazi kwenye Kambi yetu ya Avic, viongozi wa utawala na hata wasaidizi wangu kwenye benchi.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad