Laana ya Kocha Nabi Yaendelea Kuitafuna Kaizer Chiefs, Kocha Aliyechukua Nafasi yake Ashambuliwa na Mashabiki

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa


Mashabiki wa klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika ya Kusini, wamshambulia kocha wa klabu hiyo, Molefi Ntseki, baada ya kupoteza mchezo dhidi ya SuperSport United kwa bao 1-0 siku ya Jumatano.

Mashabiki hao waliojawa na ghadhabu walimrushia makopo ya maji Kocha, Molefi Ntseki aliyelazimika kutolewa uwanjani chini ya ulinzi mkali wa polisi wa kuzuia ghasia.

Hasira za mashabiki zilitokana na mwenendo mbovu wa klabu hiyo baada ya kupoteza michezo mitatu, huku ikiwa ni mara ya pili kwa mashabiki hao kumshambulia Ntseki, ambapo tukio kama hilo lilitokea wakati Amakhosi, walipopoteza dhidi ya TS Galaxy mwezi uliopita.

Kaizer Chiefs imefanikiwa kukusanya pointi 8 pekee kwenye mechi 7 ilizocheza, hivyo kujikuta nyuma kwa pointi 13 mbele ya vinara wa ligi hiyo, Mamelodi Sundowns.
_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad