Lulu Diva "Ukinipa Rich Mavoko na Maandazi Nachagua Maandazi"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Lulu Diva "Ukinipa Rich Mavoko na Maandazi Nachagua Maandazi"


Msanii Lulu Diva kutokea Bongo +255 amemdhihaki aliyekuwa mshikaji wake wa karibu msanii wa kiume Rich Mavoko kwa kusema kwamba maandazi yana thamani kuliko msanii huyo aliyebuma.


Diva ambaye alikuwa anafanyiwa mahijiano kwenye kituo cha redio cha East Africa aliulizwa kati ya Rich Mavoko kwa mkono wa kulia na maandazi kwa mkono wake wa kushoto atachagua nani, alijibu kwamba maandazi yana thamani kuliko Mavoko kwa hiyo bila kusita atachagua maandazi.


“Ukimweka mwanetu Rich na Andazi kwamba Diva anaenda kwa moja utachagua nini?” Mtangazaji alimuuliza.


“Sasa hilo si jibu liko wazi jamani Andazi. Rich Mavoko na Andazi, naendea Andazi ndugu yangu. Si kwamba kanifanya kitu kibaya lakini iko hivi, sasa mimi nikimchagua sasa hivi Rich tunaenda wapi?... Tanga? Halafu tufanyeje?” Lulu Diva alisema.


Itakumbukwa wengi walikuwa wanahisi kwamba kulikuwepo kitu Zaidi ya ushikaji baina ya wasanii hao wawili, haswa kwa vile walivyoonesha chemisty ya kudumu kwenye kolabo yao ya ‘Ona’ ya wengi walihisi wawili hao huenda waliwahi kuwa wapenzi.


Hili ni jambo ambalo hata hivyo Luu Diva alikanusha vikali alisema kwamba Rich Mavoko ni mshikaji tu ambaye kwa sasa hana thamani yoyote ya kulinganishwa na thamani ya Maandazi.


“Lakini sio katika hali mbaya, yaani tulishamaliza chochote nisme kilichokuwa kinatuweka kati yetu pamoja. Na ninaamini mimi ukiongelea Ex na Andazi, Rich Mavoko sio Ex wangu. Rich ni Mshikaji, ni rafiki yangu tuliyefanya project ya muziki ya pamoja. Kwa hiyo mimi nitachagua Andazi Zaidi ya Ex wangu lakini ukiniambia Rich kama rafiki yangu na Andazi nitamchagua Rich,” Lulu Diva alijieleza.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad