Ommy Dimpoz: Hakuna Mtanzania Atapata Show South Au Ulaya Na Atambulishwe Kuwa Ni Msanii Wa Amapiano

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Ommy Dimpoz anasema pamoja na wasanii wa Tanzania kufanya nyimbo za Amapiano kwa wingi, kamwe haitokuja kutokea wakatambulika nje ya nchi kama ni wasanii wanaofanya muziki huo.

Ommy amefunguka hayo Ijumaa hii (Septemba 8, 2023) kwenye mahojiano na watangazaji Bobby Mongi na Evans Bukuku kwenye kipindi cha Big City Breakfast cha Mjini FM.

“Haitakuja kutokea msanii wa Tanzania, hata ikitokea itakuwa once in a while, msanii wa Tanzania au Dj wa Tanzania akapata booking ya kwenda kuperform South Africa au Europe kwa kumchukulia kwamba huyu ni Dj wa Amapiano au msanii wa Amapiano kutoka Tanzania,” amesema staa huyo.

“Wakitaka msanii wa Amapiano kwenye matamasha yao watafanya booking kwa msanii wa huko huko South Africa,” ameongeza.

“Yaani mimi ninajua kuna mtu ambaye hiki kitu ndio chake, kwanini nimchukue yule anayekopi? Kwanini hawajaenda kutafuta Dj wa Singeli South Africa wamekuja straight Tanzania! Kwasababu wanajua hii ni sound original ya Tanzania. Kama wanahitaji msanii wa Taarab kwenda kuperform Europe, hawawezi kutafuta msanii wa Taarab Uganda.”

Ommy ameshauri kuwa kama wasanii wa Tanzania watahitaji kuiga vionjo vya nje, hawatakiwi kuiga kila kitu.

“Unaweza ukaiba cha mtu ukakiboresha kwa kuongeza chako,” amesema. “Kama Wanaijeria wanavyofanya, wameiona nguvu ya Amapiano, ndio maana kuna mtu kama Asake, ukimsikiliza Asake hasound kama MSouth Africa, anasound kama Mnaijeria lakini ameichukua sound ya Amapiano kaongeza na Afrobeats, kwahiyo uhalisia bado upo ndani,” amesisitiza muimbaji huyo.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad