Tin White Acharuka Kisa Rich Mavoko 'Baba zao Wanauza Karanga'

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Tin White Acharuka Kisa Rich Mavoko 'Baba zao Wanauza Karanga'

Msanii mkongwe wa vichekesho nchini, Martin Lukanga maarufu kama 'Tin White' amewashangaa wanaomsema mdogo wake, Richard Martin ambaye ni msanii wa Bongo Fleva kuwa amefuria.


Kauli hiyo ya Tin White imekuja ikiwa ni siku chache baada ya picha kusambaa zikimwonyesha msanii huyo nguli akifanya shoo ya 'Chaka to Chaka' vijijini huku maneno yakiibuka kuwa staa huyo aliyewahi kufanya kazi na lebo ya WCB amefuria na hana lolote tena.


“Wanaomsema Rich Mavoko watakuwa hawana akili kwa sababu kuna baba zao wanauza vitumbua, sigara, karanga na hawapo vizuri. Ile karanga anyaouza anafanya ili pate chochote kitu.


“Mavoko alichokifanya ni kitu kikubwa, kuonyesha kwamba anatakiwa anafanye vile. Yupo mjini miezi labda miwili hakuna shoo, sisi tukaja na wazo la 'Chaka to Chaka', mwanzoni alikuwa haielewi, lakini alipokuja kuelewa akasema hata kama kuna shoo 100 naitaka.


“Ukifika kule kuna watu mpaka 15,000 wote wanaingia kwenye hiyo stage iliyozungushiwa kamba kuja kumwangalia Rich Mavoko na anapata maokoto. Hapa Dar inaweza kuandaliwa shoo wasifike hata watu 500, lakini kule kuna mashabiki wengi, kwa nini ukatae kwenda.


“Ninachomshauri sasa hivi Mavoko aachie mangoma makali ili yaweze kuwafikia vizuri zaidi. Yale mangoma ya Kingereza a-balance kidogo ili ngoma zake zifike mpaka huko chaka watu wana mkubali.


“Akipata nafasi ya kuitwa Wasafi Festival akae chini azungumze nao kwa sababu sidhani kama kuna mtu hataki pesa, wakikubaliana fresh akapige pesa,” amesema Tin White.


Comments:

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad