Mchezaji Aziz KI Ageuka Kuwa Adui wa Makipa Bongo

 

Mchezaji Aziz KI Ageuka Kuwa Adui wa Makipa Bongo

Mtaalam wa mapigo huru ndani ya Yanga, Aziz KI amekuja na mtindo mpya kwa msimu wa 2023/24 kwa kuwavuruga makipa waliokariri ubora wake wa kutumia mguu wa kushoto kufunga.


Ikumbukwe kwamba msimu wa 2022/23 Aziz KI alitupia mabao 9 na alitengeneza pasi tano za mabao kwenye mechi za ligi.


Mabao yote na pasi hizo alizotoa katika mechi 24 alizocheza akikomba dakika 1,486 alitimiza majukumu yake kwa kutumia mguu wa kushoto na kuandika rekodi ya kuwa nyota mwenye mabao mengi kwa mguu wa kushoto.


Kibao kimegeuka msimu wa 2023/24 kawavuruga makipa wa timu mbili kwa kutumia mguu wa kulia kufunga mabao jambo lililowapa maumivu ya kuokota mpira kwenye nyavu.


Ni mbele ya KMC alifungua akaunti yake ya mabao alipopachika bao hilo dakika ya 58 akiwa ndani ya 18 kwa mguu wa kulia na bao lake la pili alifunga kwa mguu wa kulia ilikuwa dhidi ya Geita Gold.


Katika mchezo huo kipa Sebusebu Samson alipoona mpira upo kwenye mguu wa Aziz KI alijipanga kuokoa kwa kuelekea upande wa kushoto ngoma ikabadilishwa ikapigwa kwa mguu wa kulia na kumvuruga mazima.


Kibindoni ana mabao sita akiwa ni namba moja kwa utupiaji. Miongoni mwa timu ambazo kazitungua kwa mguu wa kushoto ilikuwa dhidi ya JKT Tanzania, Uwanja wa Azam Complex ilikuwa dakika ya 45 alipofunga kwa pigo la faulo.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad