Netanyahu : Israel Tunaingia Katika Vita Ngumu na Ndefu, Watu 900 Wameuawa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



TAKRIBANI Waisraeli 900 wameripotiwa kuwawa na 100 wengine kutekwa nyara katika mashambulizi yaliyoendeshwa na vikosi vya wanamgambo wa Hamas ndani ya Israel. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa iliyonukuliwa na vyombo vya habari ya serikali ya Israel, zinaeleza kuwa Waisraeli hao wameuawa tangu kuanza kwa mashambulizi hayo, jana Jumamosi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, zaidi ya watu 100 wametekwa nyara na wengine zaidi ya 2,000 wamejeruhiwa.

Hata hivyo, wanamgambo wa Hamas, wamesema leo kwamba watatoa idadi kamili ya wanajeshi na raia wa Israel wanaowashikilia mateka ndani ya saa chache zijazo.

Aidha, Hamas wamesama wataendeleza kile wanachokiita, “kulipiza kisasi kwa uvamizi wa Israel.”

Mapigano kati ya wanajeshi wa Israel na wanamgambo wa Kipalestina yaliyoanza mwishoni mwa wiki, yamesababisha umwagikaji mkubwa wa damu.

Katika eneo la Gaza, takriban watu 370 wameuawa kufuatia mashambulizi ya anga ya Israel, kwa mujibu wa maafisa wa Palestina.

Vikosi vya Israel vinadai vimeweza kuwaokoa raia wa nchi hiyo waliotekwa na wanamgambo wa Kipalestina kutoka Gaza na kurejesha udhibiti wa baadhi ya maeneo yaliyotekwa.


Jeshi lilisema kuwa wanajeshi walikuwa wamekomboa maeneo 22 kusini mwa Israel lakini bado wanapambana katika maeneo mengine manane.

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amenukuliwa akisema, taifa lake linaingia kwenye “vita virefu na vigumu.”

Ameonya Hamas, ambayo inatawala Gaza, kwamba maficho yake yatageuzwa kuwa “vifusi.”


Lakini kiongozi wa Hamas, Ismail Haniyeh, anasema kuwa wanatazamia “ushindi mkubwa” katika vita hivyo.

Wizara ya Afya huko Gaza – ambayo inasimamiwa na Hamas – inasema watu 313 wameuawa katika mashambulizi ya anga ya Israel.

Afisa mmoja aliniambia zaidi ya nusu yao ni raia. Idadi hiyo pia inajumuisha zaidi ya watoto 20 na wanawake sita, mmoja wao akiwa mjamzito.

Israel inasema inalenga nyumba za makamanda wa Hamas, lakini raia pia wametumbukizwa katikati ya mashambulizi hayo.

Kumekuwa na wito kwa Wapalestina kufika hospitalini na kuchangia damu.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad