Watano wafariki ajalini, wakiwemo mama na wanawe pacha

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Songwe. Mama mmoja na wanaye pacha wamefariki katika ajali ya lori kugonga bajaji katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma jana Jumanne Oktoba 17, 2023.

Kamanda wa Polisi Mkoani hapa ACP Theopista Mallya amesema katika ajali hiyo watu watano wamefariki dunia wakiwamo pacha na mama yao.

Kamanda Mallya amesema ajali hiyo imetokea kwenye mteremko wa Mlima Chengula eneo la Sogea Tunduma katika Barabara Kuu ya Mbeya -Tunduma na kwamba lori lililotoka juu lilimshinda dereva na kuigonga bajaji iliyokuwa na abiria.

Amewataja waliofariki ni abiria wa bajaji ambao ni mwanamke Faustina Hala (50) ambaye alikuwa na watoto wake pacha Vicent Faustin (25) na Venance Faustin (25) ambao wote wamefariki na walikuwa mafundi selemala.


Hata hivyo, amesema miili ya watu wawili ambao ni dereva wa bajaji na utingo wa lori naye haijatambuliwa kutokana na dereva wa lori kukimbia.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad