Harmonize Afunguka Ukweli Mchungu: Msiwaruhusu Wapenzi Wenu Waende Gym Peke yao

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Harmonize Afunguka Ukweli Mchungu: Msiwaruhusu Wapenzi Wenu Waende Gym Peke yao

Staa wa Bongo Fleva, Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize amewaonya wanaume dhidi ya kuwaruhusu wapenzi wao wa kike kwenda kwenye ukumbi wa mazoezi wenyewe bila kuambatana nao.


Katika taarifa yake siku ya Jumanne jioni, bosi huyo wa Konde Music Worldwide alionya kuwa wanawake wanapokwenda kufanya mazoezi kwenye gym bila wapenzi wao huanza kuwaona wavivu na wasiostahili.


Alisema kuwa katika hali kama hizi, wanawake kama hao huanza kukagua upya chaguzi zao na kuona kama watu wanaokutana nao kwenye gym kama ndio wanaolingana nao.


“Usiruhusu mpenzi wako kwenda gym mwenyewe kukiwa hakuna sababu za msingi ataanza kuona mzembe na atakaokutana nao kila siku ndio ataanza kuona bora maana wana passion moja!!,” Harmonize alisema kwenye mtandao wa Instagram.


Aliongeza; "Watabadilishana namba, kesho niamshe, taabu inaanza hapo!! Sio wote lakini, hakikisha kuwa wewe ndiye mkufunzi wake binafsi. Mnishukuru baadaye!!”


Konde Boy alisema ushauri wake ulichochewa na yaliyomtokea hapo awali, akidokeza kwamba jambo kama hilo lilitokea kwa mmoja wa wapenzi wake wa zamani.


Alidokeza kuwa uhusiano kati ya mwanamke anayeenda gym na mkufunzi wake wa kibinafsi sio wa kuaminiwa kwani lolote linaweza kutokea kati yao.


“Ukaribu wa wakufunzi na mwanafunzi ni mkubwa sana. Lolote laweza kutokea. Hawawezi kumaliza mazoezi bila kumnjoosha viungo, mara mgongo. Sio wote lakini,” alisema.


Bosi huyo wa Konde Gang hata hivyo hakushiriki maelezo zaidi kuhusu uzoefu yaliyomtendekea au kufichua ni mpenzi yupi wa zamani aliyemfanya atoe ushauri huo.


Hata hivyo, kuna uwezekano mkubwa kuwa staa huyo wa Bongo Fleva alikuwa akimzungumzia mpenzi wake wa hivi majuzi, Fridah Kajala Masanja ambaye ni mpenzi mkubwa wa mazoezi ya viungo.


Kajala huonekena mara kwa mara kwenye ukumbi wa mazoezi na hupenda kushiriki picha na video za vipindi vyake na mkufunzi wake wa kibinafsi.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad