Mkurugenzi wa Uvuvi Atumbuliwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mkurugenzi wa Uvuvi Atumbuliwa


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega ameelekeza kuondolewa katika nafasi yake Kaimu Mkurugenzi wa Uvuvi, Stephen Lukanga baada ya kushindwa kupanga na kutekeleza mikakati thabiti ya kukomesha uvuvi haramu nchini.

Waziri Ulega ametoa maamuzi hayo wakati akikabidhi boti (11) zenye thamani ya Shilingi ya Bilioni 1. 85 zilizotolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) kwa mkopo kwa wavuvi wa Mkoa wa Dar es Salaam hii leo Novemba 28, 2023.

Waziri Ulega amefika maamuzi hayo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wadau wa Uvuvi Mkoani Dar es Salaam ya kukithiri kwa vitendo vya Uvuvi haramu katika ukanda Pwani hususani Dar es Salaam.

Oktoba 4, 2023 akiwa Mkoani Mwanza katika Soko la Lumumba, Waziri Ulega alimtaka Kaimu Mkurugenzi huyo kuwa ndani ya Mwezi mmoja kuhakikisha anapanga na kutekeleza mikakati thabiti ya kukomesha uvuvi haramu nchini ambao kwa muda umekuwa ni kikwazo kwa maendeleo ya sekta ya uvuvi.

Kufuatia kushindwa kutekeleza mikakati hiyo, Waziri Ulega ameamua kumuondoa katika nafasi hiyo na kuelekeza nafasi hiyo apewe aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani, Prof. Mohamed Sheikh.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad