DC Chamwino apata ajali

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Dodoma. Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Gifty Msuya amejeruhiwa baada ya gari alilokuwa amepanda kugonga treni eneo la Iyumbu Jijini Dodoma walipokuwa wakitoka kwenye sherehe.

Sherehe hiyo iliyofanyika juzi usiku Novemba 28 ilikuwa ni kwa ajili ya kupongezana kwa Mkoa wa Dodoma kushika nafasi ya kwanza kwenye mbio za Mwenge mwaka 2023.

Mkuu huyo wa wilaya ambaye yeye na dereva wake walipata majeraha mwilini, amelazwa Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa ajili ya matibabu zaidi.

Alipoulizwa leo Novemba 30, 2023, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino, Dk Semistatus Mashimba amethibitisha DC huyo kupata ajali.


Hata hivyo, Dk Mashimba amesema hawezi kuzungumza zaidi kwa kuwa yupo kwenye kikao.

Alipotafutwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno, hakupatikana baada ya simu yake kuita bila majibu.

Hata hivyo, taarifa kutoka kwenye chanzo cha kuaminika zinasema Msuya alipata ajali hiyo saa 1:00 usiku wakati akirejea nyumbani kwake baada ya kumalizika kwa sherehe hiyo iliyofanyika mjini Dodoma.

Taarifa hizo zinasema baada ya sherehe kuisha, Gifty walitumia barabara ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ili watokee barabara kuu ya Morogoro eneo la Ihumwa, lakini wakati anavuka reli ya kati ndipo alipogonga treni.

"Alikuwa na dereva wake, bahati mbaya wakati wanavuka daraja la reli ya mwendo kasi ndipo walipopata ajali maana waligonga treni waliyokutana nayo wakati wanavuka,” kimesema chanzo hicho.

Chanzo hicho kimesema hali ya DC huyo inaendelea vizuri kwa sababu pamoja na kuumia, hakupata majeraha mabaya isipokuwa michubuko na maumivu kidogo ambayo yamesababisha alazwe kwa uangalizi zaidi.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad