Serikali Yachukua Hatua za Awali Kukabili Maafa Hanang’

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Serikali Yachukua Hatua za Awali Kukabili Maafa Hanang’


Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu imechukua hatua za haraka kwa wahanga wa maafa yaliyosababishwa na maporomoko ya tope yaliyotokea tarehe 03 Disemba, 2023 ambapo yalitoka mlima Hanang uliopo Mkoa wa Manyara na kusababisha vifo vya watu, majeruhi na uharibifu mkubwa wa miundombinu mbalimbali yakiwemo mashamba, na makazi ya wananchi wa eneo hilo.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonazi pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wamefika katika kijiji cha Gendabi kata ya Gendabi Wilaya ya Hanang’ mkoani Manyara eneo yalipotokea maporomoko ya tope jana tarehe 04 Disemba 2023.


Viongozi hao wameongozwa na Mkuu wa Mkoa Manyara Mhe. Queen Sendiga kufika katika Kijiji cha Gendabi ambalo ni eneo liliothirika Maporomoko ya tope kutoka Mlima wa Hanang yaliyotokea usiku wa kuamkia tarehe 03 Disemba 2023.


Akiwa eneo la tukio hilo, Waziri Mhagama, amewaomba wananchi hao kupokea pole ambazo zinatoka kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ambaye aliagiza lazima KUfika eneo la tukio na kuona nini kifanyike kwa dharura kuhusu uokoaji pamoja na makazi kwa waathirika hao.


“Mambo haya yakitokea kuna mambo ya haraka yanatakiwa yafanyike kwa dharura hivyo tumekuja na kushauriana namna ya kujipanga kwa pamoja ili kufanikisha jambo hilo kwa uharaka”. Ameongeza Mhagama


Ameongeza kuwa, maelekezo ya Mheshimiwa Rais kwanza kuona namna gani wanaweza kuendelea kuokoa watu na kazi hiyo wanaendelea nayo vikosi vya uokoaji, pia kuangalia namna gani ya kuweza kuwasitiri wenzetu waliotangulia mbele ya haki.


Aidha, Waziri Mhagama amesema kuwa Serikali imeshaleta wataalamu wa Miamba watatoa taarifa ya nini kilichotokea na nini kifanyike katika mlima wa Hanang.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad