Watanzania 500 Kuajiriwa na Serikali ya Saudi Arabia, Tuma Maombi yako Hapa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetangaza ajira 500 za Wauguzi wa kike ambao wataajiriwa na Serikali ya Saudi Arabia mapema mwezi January mwaka 2024.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea na dhamira yake thabiti ya kuhakikisha Watanzania wananufaika na fursa za ajira zinazojitokeza kutokana na mahusiano mazuri yaliyopo baina ya Tanzania na Mataifa mbalimbali duniani.


Mhandisi Luhemeja amesema hivi karibuni mwishoni mwa mwezi November na mwanzoni mwa mwezi December, 2023, Serikali ya Tanzania imesaini hati mbili za makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya kazi na ajira na Serikali ya Saudi Arabia pamoja na Serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu.


Amesema hati za mashirikiano zilizosainiwa zinatoa fursa za ajira kwenye Mataifa husika kwa kada na sekta zenye kutumia ujuzi wa chini, ujuzi wa kati na ujuzi wa juu.


Amesema Watanzania wote wenye sifa na ujuzi uliobainishwa wanataarifiwa kuomba kazi husika kwa kujisajili https://jobs.kazi.go.tz na kutuma wasifu binafsi (CV) kwa njia ya barua pepe esu@taesa.go.tz ambapo mwisho wa kutuma maombi ni December 27 2024

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad