Teuzi Mpya Zanzibar, Huyu Hapa Aliyechukua Nafasi ya Waziri Aliyejiuzulu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amefanya mabadiliko ya Baraza la Mapinduzi kwa kuteua
Mawaziri wapya wawili na kumbadilisha Wizara Waziri mmoja ambapo amemteua aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Mudrik Soraga kuwa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, akichukua nafasi ya Simai Mohamed Said aliyejiuzulu.

Katika uteuzi huo, Dkt. Mwinyi pia amemteua Ali Suleiman Ameir (Mrembo), kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Ikulu ambaye awali alikuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango na kumteuwa Shaaban Ali Othman kuwa Waziri wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi ambapo awali alikuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini.

Wengineni Juma Makungu Juma, ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi, wakati Salha Mohamed Mwinjuma ameteuliwa kuwa Naibu Waziri
wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi, akiachia nafasi yake ya uwakilishi wa Viti Maalum kutoka Kundi la Vijana Kusini, Unguja.

Aidha, Dkt. Mwinyi pia amemteuwa Zawadi Amour Nassor kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini, ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Konde, Mkoa wa Kaskazini, Pemba huku taarifa ya Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Said ikieleza kuwa, uteuzi huo unaanza hii leo Januari 27 , 2024 na Viongozi walioteuliwa wataapishwa baadaye
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad